WAKAAZI WA SHEHIA YA URUSI WAITAKA SERIKALI KUWASAIDIA VIJANA WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA

 

Wakaazi wa shehia ya urusi wametaka juhudi zaidi zichukuliwe kusaidia vijana  kuacha kutumia dawa  za  kulevya  zinazowafanya kushiriki katika vitendo  viovu  vikiwemo  vya  udhalilishaji.

Wamebainisha  hayo  katika  kikao  cha  shehia  kilichowashirikisha kikundi  cha daawa  kutoka  kitengo  cha  wanawake  na  watoto  cha  wilaya  mjini, kilichojadili njia mbadala za kupambana na vitendo  hivyo vinavyozidi  kushamiri  kila siku.

Wamesema vitendo hivyo vinachangia kukosekana nguvu  kazi  ya taifa kutokana na  vijana wengi kupoteza mwelekeo wa kimaisha, kuharibu mali  za watu na kujishirikisha na vitendo vya udhalilishaji kwa  wanawake  na watoto.

Nao kitengo cha utoaji  daawa wamesema hakuna budi kurudisha  malezi shirikishi  katika  jamii  ili  kuwa  na mpango  utakaowawezesha   vijana kuwa na maadili  mema.

Sheha  wa  shehia  hiyo  ya  urusi  yusuf juma  mtumwa  ameahidi  kushirikiana na wakaazi  wa  shehia  yake  kutoa  taarifa  mapema  wanapoona ishara ya vitendo vya uvunjifu  wa  maadili kabla  kuwaletea  madhara.