WAKAAZI WALIOJENGA KATIKA HIFADHI YA MAJI YA MAKUFULI WAMEPEWA WIKI MOJA KUHAMA KATIKA HIFADHI HIYO

 

wakaazi waliojenga katika hifadhi ya maji ya makufuli shehia ya welezo wilaya ya magharibi a wamepewa wiki moja kuhama  katika hifadhi hiyo na kupisha mradi mkubwa wa maji safi katika eneo hilo ambao utasambaza maji katika maeneo mengi ya unguja.

mkurugenzi wa halmashauri magharibi “a” nd. amur ally musa amewasisitiza wakazi hao kuhama ili kutokwamisha mradi huo wa maji na kuwataka wenye leseni za ujenzi kuzipeleka halmashauri kwa hatua zaidi.

naye msahiki meya baraza la manispaa magharib a ndugu hamza khamisi juma amesema mradi huo una manufaa kwa wazanzibar wote hivyo ni vyema kwa wakaazi hao kufuata maelekezo waliyopewa kuufanikisha.

naye afisa uhusiano wa mamlaka  ya maji zawa ndugu zahoro suleimani khatibu amewaomba wananachi kufuata taratibu za ujenzi na kuacha kujenga katika vyanzo vya maji kwani wanakwamisha miradi ya maji safi na salama.