WAKALA WA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR IMEKAMATA MADUMU 747 YA MAFUTA

 

Wakala   wa  chakula  dawa  na  vipodozi  zanzibar  imekamata  madumu  747 ya mafuta  ya  kupikia aina  ya  turkey yakiwa  katika  zoezi  la  ubadilishaji  wa nembo  kwa  kutoa  ya  turkey  na  kuweka  ya  ok  ambayo  nayo  ni  ya  kughushi   kitendo  ambacho  ni  kinyume  cha  taratibu  kilichofanyika  ndani ya  tawi  la  ccm  makadara.

Akizungumza  na  waandishi  wa  habari   kaimu  mkurugenzi mtendaji  wa  wakala  wa  chakula  dawa  na  vipodozi  zanzibar  na mdhibiti  wa  chakula  na  dawa  dk  khamis  ali   amesema  kitendo  hicho  nicha  ubadhirifu kinacholenga kuwababaisha  mlaji  kutumia bidhaa  asiyoikusudia.

Amesema kitendo  hicho  kwa  mujibu  wa  sheria  hakistahiki  kwani  kinaweza  kuharibu soko  la  bidhaa  moja  kwenda  nyingine  kutokana na udanganyifu unaofanywa na  wafanyabiashara na  kusababishia  kutumika  kwa  bidhaa   zisizofaa  kwa  jamii .

Mwakilishi wa kampuni  ya  sahara  trade  ambae  ni    mmiliki  wa  nembo  sahihi  ok   salum  humudi  amelaani  vitendo hivyo vinavyofanywa  na  baadhi  ya  wafanyabiashara  kwani vinaweza  kuharibu  soko  halisi  la  bidhaa  yao ambako  kunaweza  kushuka soko  lao  kiuchumi  kutokana  na  wananchi  kupata  huduma  wasioitarajia.

Nae  katibu  wa  ccm  jimbo  la   malindi  ambalo  linalomiliki  tawi  hilo ndsalum  juma amesema chama  hakihusiki  kwa  kuwepo  kwa  bidhaa  hiyo  ndani  ya  tawi  lake na  kutaka sheria  za  kinidhamu  zitachukuliwa  kwa  aliehusika  na kadhia hiyo.

Madumu  hayo  ya  lita  20  yakiwa  747 yakitolewa  ndani  ya  tawi  hilo  vikiwa  pamoja  na  vifaa  vilivyotumika kubadilishia nembo  hizo  mali  yaa ujudi  abasi ambae  amesema  ameazima  eneo  hilo  kwa  kuweka  bidhaa  yake.