WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR IMEKAMATA BIDHA MBOVU

 

Wakala wa  chakula  na  dawa  zanzibar  imekamata  bidha  mbovu  ambazo  hazifai kwa  matumizi  ya  binaadamu  jumla  ya  tani 40  za  mchele ,unga  wa  sembe 75,25  za  sukari,tani tisa za  vipodozi   na  lita  15  za  mafuta ya  kula  yaliokuwa  yakibadilishwa  nembo  kwa  maana  ya  kughushi  kwa  kufanya udanganyifu kwa  wateja.

Akitoa  tathmini  ya  utendaji  wa  kazi  zao  katika  kipindi  cha  miezi miwili kupitia  ukaguzi madukani  na  maeneo  ya bandari  na  uwanja wa ndege   mkurugenzi  mtendaji  wa  wakala  wa  chakula  na  dawa  zanzibar  dk  burhani  othman  simai  amesisitiza  wanaotoa  misaada  kwa  jamii  kutoa taarifa wakala ili  kuthibitika  ubora  wa  bidhaa hizo  kwa  lengo la  kulinda  afya za  mlaji  kutokana na  kisingizio waliowengi  kutoa  msaada  katika  kipindi  cha  mwezi  mtukufu  wa  ramadhani.

Amesisitiza  wafanyabiashara  kuacha udanganyifu  katika  uingizaji  wa  bidhaa  na  kuitumia  wakala  wa  chakula  na  dawa  ili kuweza  kuleta  bidhaa  zenye  tija  na mahitaji nchini  kwa kutambua  viwanda  vyenye  viwango  vya  uzalishaji  wa  bidhaa  hizo.

Ameitanabahisha  jamiii  kutoa  ushirikiano  zaidi  na  wakala  huyo  kwa  kutoa  taarifa mapema   pindipo  wanapoona  bidhaa  wenye  kuzitilia  mashaka  na  kuachana  na  habari za  utotoshaji  zinazorushwa  mitandaoni  zenye  lengo  la  kuwaletea  taharuki  kwani  serikali  yao  kupitia  wakala huyo wapo  makini  katika  kumlinda mlaji.

Kutokana  na bidhaa  hizo  zilizokamatwa  katika miezi  miwili  hiyo katika maeneo  tofauti likiwemo  ghala  la muhammed  matar,ryto phamacy iliyopo darajani  wahusika washafikishwa  katika  vyombo  vya  sheria ikiwa  sambamba na kugharamia  gharama za  uangamizaji.