WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR IMETEKETEZA JUMLA YA TANI 6 NUKTA 5 ZA SAUSAGE

Wakala wa chakula na dawa zanzibar imeteketeza jumla ya tani 6 nukta 5 za sausage zilizopitwa muda wa matumizi ambazo zinaweza kuleta athari ya kiafya kwa binaadamu.
mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji wa madhara ya chakula aisha suleiman amesema bidhaa hiyo imekamatwa katika ghala la kampuni ya best import iliyopo maruhubi baada kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Amefahamisha kuwa upo umuhimu kwa wafanyabiashara wa chakula kuhakikisha usalama wa bidhaa zao kabla ya kuingiza nchini ili kuzingatia afya za walaji.
Mkaguzi wa chakula amina ramadhan ameisisitiza jamii kuwa makini na bidhaa wanazozinunua pamoja na kuzidisha ushirikiano nao pindipo wakibaini uingizwaji au usambazwaji wa bidhaa ambazo wanazitilia mashaka kwa afya za binaadamu.
Utaratibu wa kuteketeza bidhaa zisizofaa kisheria no 2 ya mwaka 2016 na marekebisho yake no 3 2017 kwa wakala wa cchakula na dawa zanzibar kuteketeza bidhaa zilizopitwa na muda ama zisizofaa kwa matumizi ya binaadamu au kurejesha mzigo ulikotoka chini ya gharama ya mmiliki.