WAKATI MVUA ZA MASIKA ZIKIENDELEA KUNYESHA WANANCHI WAMETAKIWA KUENDELEA KUFANYA USAFI

 

Wakati  mvua za masika  zikiendelea kunyesha  wananchi wametakiwa kuendelea kufanya  usafi katika mazingira  wanayoishi ili   kuepuka  maradhi ya mripuko hasa kipindupindu. Mratibu wa kijiji cha SOS Ndugu Juma Hamad  akizungumza kwa nyakati tofauti na  baadhi ya wananchi wa Shehia ya Mombasa  walipokuwa wakifanya usafi katika  maeneo yao   amesema suala la usafi  ni muhimu nalinaweza kuwasaidia  katika kupunguza gharama za matibabu.amesema wananchi wasifanye mzaha kuimarisha usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi sambamba  kuzuwia watoto kuchezea maji machafu  na kuchemsha maji  kabla ya kuyatumia.kwa upande wake mwenyekiti wa vijana shehia ya mombasa Ndugu Iddi Haji Rajab, amewaomba vijana wezake   kujitolea kwa kufanya usafi ili kulinda  afya zao na familia zao  kwa jumla

Sheha Shehia hiyo ndugu  Hussein Abrahman Yussuf, amesema suala hilo wameliweka mikakati  ya kulitekeleza  kila ifikapo mwisho wa mwezi katika shehia yao ya mombasa na amewashukuru wnanchi wake kwa kujitokeza katika zoezi  hilo pamoja na kuiomba serikali kuwasidia vifaa vya kufanyia usafi.