WAKATI SASA UMEFIKA WA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA WATU WANAOJENGA KIHOLELA SEHEMU ZINAZOKAA MAJI

Kammisheni ya maafa ikishirikianana watu wa ardhi na makazi bora wamefanya zoezi la kukagua maeneo hatarishi ya makaazi ya wananchi waliojenga katika sehemu zinazokaa maji kwa ajiliya kuchukua tahadhari ambapo mvua za vuli zinazoendelea kunyesha ili kujiepusha na majanga.
Zoezi hilo limefanyika katika sehemu mbali mbali za mabondeni zinzokaa maji sebleni pamoja na nyerere mwatenga a na b.
afisa ardhi ndugu wahidi zahrani nassor amesema si ruhusa kwa mtu yoyote kujenga nyumba katika maeneo hatarishi kwa hivi sasa imekua watu wanachukua uwamuzi wa kujenga nyuma bila kupewa kibali jambo ambalo ni kosa kisheria na tayari wamesha fanya tadhmini watu walio ruhusiwa kujenga mbali na bonde hilo ambapo imeonekana watu hawachukuliwi sheria ndio wanajenga kiholela .
Naye afisa operesheni misaada ya kukabiliana na maafa shaabani hassan ramadhani amesema wakati sasa umefika wa kuchukuliwa hatua za kisheria watu wanaojenga kiholela na kusema kuna baadhiya watu hulima bustaniya mboga mboga na baadae hujenga nyuma kwa ajili ya makaazi ya kudumu kwa kupuuza sheria za nchi .
nao wakaazi wa maeneo hayo bi fatma ali na mgeni ramadhan wamesema kipindi cha mvua wamekua wanapata shida ya kuhama na watoto na hata kusababisha vifo kwa watoto wadongo.
sheha wa shehia ya sebleni juma ramadhan amesema kuna baadhi ya watu huchimba mchanga maeneo ya mabondeni nyakati za usiku na kusababisha waafa kwa watoto wanaoogelea sehemu hizoa na kuiomba serikali kuchukua tatua.