WAKATI UMEFIKA KUTAFAKARI NA KUPANGA KUANZISHA SACCOS

 

Naibu katibu mkuu wizara ya kazi uwezeshaji wazee vijana  wanawake na watoto  bi mauwa makame rajab amesema wakati umefika kutafakari na kupanga kuanzisha saccos kubwa za wilaya.

Akifunguwa warsha kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo mhe, modeline castico katika ukumbi wa wizara ya habari bi mauwa amesema mpango huo utasaidia kujenga mitaji mikubwa na imara pamoja na kuviunganisha vyama vya uzalishaji .

Nae mkurugenzi wa idara ya vyamavya ushirika zanzibar daudi khamis simba amesema baadhi ya saccos hazikidhi mahitaji na zinahitaji kupewa msukumo ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa upande wao washiriki wa warsha hiyo wameshauri mafunzo hayo yaendelee kutolewa kwa wanachama wa saccos.

Warsha hiyo ya siku moja imetayarisha na wiraza   ya kazi uwezeshaji wazee,vijana wanawake na watoto kupitia mwarfimezungumzia usimamisi na uendeshaji wa wa saccos kubwa za wilaya na mageuzi katika vyama vya kilimo.