WAKINA MAMA WATAKIWA KUWA NA MSHIKAMANO KATIKA HARAKATI ZA KUFIKIA MAENDELEO YA KWELI.

Mwakilishi wa jimbo la kijitoupele  Mh Ali Suleiman Shihata amewataka akinamama wa melinne bondeni kuwa na mshikamano na maelewano katika harakati za kufikia maendeleo ya kweli.

Mh Shihata ameeleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya melinne bondeni ambayo ni juhudi za kikundi cha akinamama wa eneo hilo.

Mwakilishi huyo  amesema hatua za akinamama hao za kusimamia maji upatikanaji wa huduma hiyo zinaonesha kuiunga mkono serikali katika harakati za kuwaondoshea kero ya maji wa wananchi wote unguja na pemba  .

Akitoa maelezo juu ya upatikanaji wa huduma hiyo mmoja wa akinamama katika maeneo ya melinne bondeni Bi Asha Diwani amesema walijikusanya baada ya kuona  wanakosa huduma hiyo kwa muda mrefu na hivyo kukamilisha taratibu kupitia zawa za kuweza kujikwamua na usumbufu wa maji.

Umoja wa akinamama hao umeweza kuyatoa maji katika laini ya maji inayotoka katika kisima cha kwerekwe c na kuyafikisha katika maeneo yao hayo kwa jitihada zao na viongozi wa jimbo hilo

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App