WAKIZUNGUMZA KATIKA MAFUNZIO YA WAZAZI WENYE WATOTO NJITI

 

 

Wizara ya afya  imewahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutoa elimu  jinsi ya kuwatunza watoto waliozaliwa kabla ya kutimiza miezi saba ambao wanaonekana kuongezeka nchini kutokana na  matatizo mbali mbali.

Wakizungumza katika mafunzio ya wazazi wenye watoto hao huko Kivunge wauguzi wakunga ndugu Ruzuna Abdulkadir na ndugu Christy harrison wamesema katika  kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa  serikali imeamua  kuanzisha  klinik za  watoto hao  unguja na pemba ili kupunguza vifo vya watoto hao

Wamesema wameamua kutoa mafunzo hayo kufuatia kuwepo  idadi kubwa ya watoto njiti wanaozaliwa hapa nchini huku wakiwasisitiza wazazi kuwa waangalifu wakati wanapowalea.

Baadhi ya wazazi wenye watoto hao wameelezea changamoto  zinazowakuba wakati wa kuwatunza watoto hao ikiwemo ile ya  uhaba  wa wauguzi katika cliniki  zao.

Zaid ya watoto kumi na nne wa walipimwa wakati wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na  taasisi ya hips .

Mafunzo hayo ni sehemu ya  maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunini ambayo huadhimishwa kila ifikapo  tarehr 17  novemba kila mwaka.