WAKULIMA WA BONDE LA KILOMBERO WAMELALAMIKIA HATUA YA WAMILIKI WA ENEO HILO KUTAKA KUWAONDOA

Wakulima wa bonde la kilombero mipirani wamelalamikia hatua ya wamiliki wa eneo hilo kutaka kuwaondoa katika eneo wanalolima na kupewa muwekezaji wa kiwanda cha sukari mahonda ili aendeleze kilimo cha miwa.
Wamesema kwa muda mrefu eneo hilo wanalitumia kwa kilimo hivyo kuondoshwa kwao kutawasababishia kukosa mahitaji muhimu ya kujikimu na familia zao.
Wamesema sera ya serikali inawataka wananchi kujiajiri wenyewe lakini kitendo cha kuondoshwa katika eneo hilo ni kwenda kinyume na sera hiyo.
Mkuu wa wilaya ya kaskazini “b” issa juma ali amesema eneo la kilombero mipirani linamilikiwa na chama cha mapinduzi na kwa sasa wameamua kulichukuwa na kutaka kulikodisha kwa mwekezaji huyo hivyo amewataka wakulima hao kuwa wastamilivu na serikali itawasimamia kupata stahiki zao na kuwatafutia eneo jengine la kuendeleza shughuli zao za kilimo.