WAKULIMA WA MATUNDA WAPEWA MAFUNZO JUU YA KUSARIFU MATUNDA HAYO

 

Wakulima wa zao la matunda na mboga mboga wamesema mazao wanayozalisha hayatoharibika shambani na kupata bei ndogo kutokana na taaluma walioipata ya kusarifu matunda hayo mara yanapokomaaWamesema muda mrefu huzalisha matunda na mboga mboga kama vile mchicha pamoja na tungule ambayo huzalisha kwa wingi na kukosa wateja na hivyo kuharibika shambani hali ambayo mkulima hafaidiki na jasho lake

Wakizungumza na zbc katika mafunzo hayo yaliofanyika katika kituo cha kusindikia matunda huko pujini chake chake pemba wakulima hao wamesema kwa sasa hawana wasiwasi juu ya mazao watakao zalisha hasa tungule kwani wana uwezo wa kuyasarifu na kuongeza thamani ambayo itawapatia tijaKwa  upande afisa kiungo katika program ya assp asha omar faki  amesema lengo la mafunzo hayo ni baada ya kuona wakulima wanazalisha kwa wingi lakini tija yao ndogo kulingana na matarajio yao

Akielezea juu ya mafuzo aliyoyatoa kwa wajasiri amali hao bi fatma mohd mzee amesema usindikaji wa bidhaa hizo ni waubora na kuwataka kuzalisha bidhaa hizo kwa wingi .Nao maafisa kilimo wamesema mafunzo hayo yatakuwa mkombozi endapo wayayatumia ipasavyo