WAKULIMA WA MWANI ZANZIBAR KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI

Waziri wa biashara, viwanda na masoko balozi Amina Salum Ali, amewashauri  wakulima wa mwani zanzibar kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao hilo huku serikali ikiendelea na mikakati ya kutatua changamoto zinazowakabili katika kilimo hicho.

Akizungumza katika shamra shamra ya kuelekea siku ya mwani duniani amesema kuwa zao hilo limekuwa na tija katika jamii kwenye masula ya biashara na kwamba serikali inajitahidi kuwawezesha wakulima wake.

Amesema zao la mwani lina mchango mkubwa wa kibiashara katika kukuza uchumi kwa mtu mmoia mmoja na taifa kwa jumla

Amefahamisha kuwa serikali inampango wa kutoa elimu ya kilimo kupitia wataalamu  na kutafuta njia za kuwapatia soko la nje na ndani ya nchi.

kuwataka wakulima hao kujitahidi na kwamba wizara itahakikisha bei ya zao hilo imaimarika na kuwanufaisha wakulima hao.

Katibu mkuu wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi, anaeshughulikia mazingira DK Islam seif amesema licha ya zao hilo kukabiliwa na matatizo lakini wizara itajitahidi kuimarisha zao hilo kwa kiwango kikubwa.