WAKULIMA WA VITUNGUU MAJI WANAKUSUDIA KUZALISHA ZAO HILO KIBIASHARA

Wakulima wa zao la vitunguu maji katika kijiji cha Makunduichi wanakusudia kuanza kuzalisha zao hilo kibiashara baada ya kufanikiwa katika mradi wa majaribio.
Wakizungumza wakati wa uvunaji wa zao hilo wanakikundi cha dhulma si njema wamesema moja ya mkakati waliouweka ni kutanua eneo la kilimo ilikuzalisha kwa wingi.
Wamesema wanaamini kuwa hiyo itakuwa njia muhimu katika kujiinua kichumi na kuondokana na umasikini.
Waziri wa nchi afisi ya rais katiba sheria utumishi wa ummana utawala bora Mh: Harouna Ali Suleiman amewataka wananchi kutokata taamaa katika kukuza vipato vyao.
Mradi huo unaendeshwa kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini wa tasaf awamu ya kwanza ambapo kikindi hicho kinawanufaisha karibu watu hamsini wa kijiji cha Makunduchi.