WAKUU WA MAJESHI YA UTURUKI, MAREKANI NA URUSI WAKUTANA.

 

Mkuu wa majeshi ya uturuki anakutana na wenzake wa marekani na urusi katika mkoa wa kusini mwa uturuki wa antalya ili kujadili kuhusu usalama wa kikanda, hasa katika nchi nchini syria na iraq.

Mwezi agosti, wanajeshi wanaoongozwa na uturuki walianzisha operesheni ya kulifurusha kundi la dola la kiislamu kutoka mpaka wa uturuki na syria na kuwazuia wapiganaji wa kikurdi kulikamata eneo hilo.

Uturuki inaliona kundi hilo kuwa sehemu ya chama cha wafanyakazi wa kikurdi – pkk ambacho kinaendesha uasi nchini uturuki.