WAKUU WA MITIHANI YA TAIFA YA ZANZIBAR KUWA MAKINI KWA UDANGANYIFU WA WANAFUNZI.

Afisa mdhamini wizara ya elimu na Mafunzo ya amali pemba salum kitwana sururu amewataka wasimamizi wakuu wa mitihani ya taifa ya Zanzibar  kuwa makini kuhakikisha hakufanyiki udanganyifu kwa wanafunzi.

Mdhamini kitwana umetowa wito huo ukumbi wa mikutano skuli ya fidel castro kwenye kikao elekezi juu ya usimamizi wa mitihani ya taifa ya zanzibar kwa wasimamizi wakuu na wasaidizi wa vituo vya mitihani na walimu wakuu.

Amesema mitihani ya zanzibar imeshuka hadhi yake kutokana na wasimamizi na walimu kushirikiana na makundi ya watu kufanya ukopiaji wa wanafunzi kitendo ambacho kinashusha uwezo wa mwanafunzi anapoendelea na masomo yake.

Mratibu wa baraza la mitihani pemba haji fakih amewakumbusha wasimamizi kuyatembelea madarasa ya mitihani mara kwa mara na sio kubakia ofisini kwani ni udanganyifu wa mitihani unaweza kutokea.

Mitihani ya taifa ya zanzibar inatarajiwa kufanyika jumatatu ya tarehe 20 mwezi huu ambapo jumala ya wanafunzi 41,790 watafanya mitihani ya kidato cha pili, darasa la saba, sita na nne.