WALIMU KUJIENDELEZA KITAALUMA KATIKA SOMO LA KIINGEREZA ILI KUENDANA NA MABADILIKO

 

 

Upo umuhimu mkubwa kwa walimu  kujiendeleza kitaaluma katika  somo la kiingereza  ili kuendana na mabadiliko na kupata mbinu mpya ya ufundishaji.Mwenyekiti wa jumuiya ya walimu wa somo la kiengereza ndugu  mkombe juma na mjumbe wa taasisis hiyo wakizungumza katika mafunzo ya uwelewa wa ufundishaji wa mbinu za lugha ya kiingereza  wamesema iwapo walimu watafanya vizuri katika ufundishaji wa somo hilo litawarahisisha wanafunzi kufanya vizuri  katika masomo yao.

Wamefahamisha kuwa lengo la mafunzo hayo kwa walimu wa somo hilo ni kuhakikisha wanapata mbinu mbali mbali za ufundishaji  ili vijana maskulini wanufaike.Baadhi ya washiriki kutoka zanzibar na tanzania bara wameziomba   serikali zote mbili kuendelea kuwaunga mkono walimu  katika mafunzo mbali mbali ili kuweza kuendeleza sekta ya elimu .Mafunzo ya ujenga uelewa kwa walimu wa somo la kiingereza kutoka skuli za sekondari na priymaryi yametolewa na wakufunzi wanaosaidia usomeshaji wa lugha ya kingereza kutoka nchini marekani .