WALIMU KUONGEZA KASI YA UFUNDISHAJI ILI KIWANGO CHA UFAULU KWA WANAFUNZI KUONGEZEKA

 

Kamati ya madiwani halmashauri ya wilaya kusini imewataka walimu wa skuli za wilaya hiyo kuongeza kasi ya  ufundishaji ili  kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika mitihani ya taifa kiongezeke.

Wakizungumza na walimu na wanafunzi wa skuli za mtule na paje wakati wa  ziara maalum  ya kuangalia  maendeleo ya elimu skuli za halmashauri hiyo wajumbe hao wamesema  kufanya vibaya kwa baadhi ya skuli  katika mitihani ya taifa mwaka  uliopita kumetokana na baadhi ya walimu kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Aidha amefahamisha sababu nyingine ni baadhi ya wanafunzi kujingiza katika vitendo viovu ikiwemo mapenzi katika umri mdogo na kujiingiza na matumizi ya dawa za kulevya .

Baadhi ya walimu na wanafunzi wa skuli ya sekondari mtule wamesema miongoni mwa mtatizo yanayoikabili skuli yao ni kuvuja kwa majengo  ,kukosa walimu wa somo la kompyuta ,huduma ya maji safi na salama  na usafiri wakati wa kwenda na kuondoka skuli.

Mustafa mohamed pochi ni mwenyekiti wa kamati ya madiwani wa wilaya ya kusini unguja amesema  wakati umefika sasa kwa wilaya kusini kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu na kuiishauri serikali kuhakikisha inatafuta wakandarasi majengo  wenye viwango.