WALIMU NA WAZAZI WAMETAKIWA KUZIDISHA JUHUDI KATIKA KUONGEZA KASI KATIKA UFUNDISHAJI WA WANAFUNZI

Walimu na wazazi pamoja na kamati ya skuli wametakiwa kuzidisha juhudi katika kuongeza kasi katika ufundishaji wa wanafunzi kwa kuhakikisha wanafaulu vizuri katika masomo yao.
akizungumza na walimu na kamati hiyo mwakilishi wa jimbo la tunguu mh: simai mohamed said amesema elimu ndio ufunguo wa maisha kwa vijana hivyo lazimz litiliwe mkazo ili taifa liweze kuendelea.
katika skuli hiyo mwakilishi simai ameahidi kuchangia zaidi ya shilingi milioni moja kwa ujenzi wa banda la skuli hiyo ambalo halijakamilika kwa sasa kutokana na nguvu za wananchi na viongozi wa taifa .
Aidha mh: simai amemkabidhi zawadi mwanafunzi mmoja aliyefaulu michipuo na kwenda skuli ya biashara ndugu rahma mustafa.
Katika risala ya walimu hao wamesema wanakabiliwa na ukosefu wa viwanja vya michezo madhi ya madarasa hayana madirisha ukosefu wa kuzingia kuta ili kujikinga na maadui .
Wakati huo huo mwakilishi huyo na mbunge wa tunguu mh: khalifa salim ameahidi kuweka kifusi katika skuli ya imani ili kupunguza matope hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea.