WALIMU WA SKULI YA BUBUBU WAMETAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII

 

Mkuu wa  wilaya ya magharib ‘a’ kapten khatib khamis  amewataka walimu wa skuli ya bububu sekondari  kufanyakazi kwa  bidii ili  kuongeza kiwango cha  ufaulu  katika skuli hiyo.Kapten  khatibu amesema  hayo  wakati wa  ziara ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo  na changamoto  katika skuli hiyo ikiwemo ujenzi wa  madarasa  na uhaba wa vikalio .  Amesema  serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi  katika kuimarisha sekta ya elimu ili kuhakikisha  wanafunzi  wanasoma katika mazingira bora  hivyo ni jukumu la walimu  kwenda sambamba na azma ya serikali kufanikisha malengo yake.

Mwalimu mkuu wa skuli ya bububu bw, said hemed nassoro  amesema kwa kushirikiana na uongozi wa kamati na wazazi wa wanafunzi wa skuli hiyo  wameweza kujenga mabanda mawili ya kusomea na kufanikiwa kuyaezeka.Naye mkurugenzi wa  manispaa  ya wilaya ya magharibi  a ndugu said  juma  ahmada  amesema  uongozi wa  manispaa  kwa kushirikiana  na baraza la manispaa magharibi a  uko tayari  kusaidia  sehemu  ya ujenzi  katika skuli  hiyo ili kuwaondoshea usumbufu wanafunzi.Mapema  katika  risala ya skuli hiyo   iliyosomwa na  mwalimu  bimkubwa  abdulrahman  imesema mbali na mafanikio yaliyopatika bado wanakabiliwa na  changamoto ya maabara.