WALIMU WA SKULI YA KISWANDUI WAMEUOMBA UONGOZI WA JIMBO LA KIKWAJUNI KUKIONDSHA KITUO CHA DALADALA

Walimu wa skuli ya kiswandui wameuomba uongozi wa jimbo la kikwajuni kukiondsha kituo cha daladala kiliopo karibu na eneo la skuli hiyo ambacho kimekuwa kikihatarisha usalama wa  maisha yao na wanafunzi.

Wakitoa malalamiko hayo kwa diwani wa wadi ya kikwajuni wamesema  kituo hicho kunachangia kutokea kwa ajali kutokana na skuli hiyo kuwepo kwa baadhi ya walimu na wanafunzi wenye mahitaji maalum  ambao hupata usmbufu wakati wa kuvuka na  akiwafariji wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma skuli hiyo diwani wa wadi ya kikwajuni ibrahim khamis fataki,amesema ni vyema kwa jamii kuwajali watoto hao na kuacha tabia ya kuwafungia majumbani na kuwaksesha haki zao za msingi ikiwem elimu.

Sheha wa shehia ya kiswandui Abass Kimoto amesema katika kutatua kero hiyo ya kituo cha daladala almewaita Madereva na Makonda wanaohusika katika eneo hilo ili kuzungumza kwa pamoja lakini walikaidi agizo hilo.