WALIMU WA SKULI ZA BINAFSI WAMETAKIWA KUFUATA MASHARATI NA MIONGOZO YA SERIKALI

 

 

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali  mh riziki pembe juma amewasisitiza walimu waskuli za binafsi kufuata masharati  na miongozo iliyowekwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar katika kuimarisha elimu ya sekondari namsingi kwa wanafuzi ili kuongezakiwango cha ufaulu nchini.

Mh riziki pembe juma ameyasema hayo wakati wa sherehe ya kuwakabidhi wanafunzi waliofaulu kidatu cha sita katika skuli ya alhisaan iliyopo mkwanakwerekwe

Amesema skili hiyo mwaka huu imejitahidi kutoa wanafunzi thalathini na moja kwa ajili ya kujiunga na elimu ya juu hivyo lazima skuli zate  za binfsi  wazingatie  sheria na kanuni walizopangiwa na serilali ili kuondosha matatizo yanayojitokeza katika utendaji wa kazi  kwakufuata  mitaala  nakuhakikisha wanafundisha kwa kuchukua  juhudi  na sio kufanya biashara .

Aidha amewapongeza walimu na wanafunzi kujitahidi sana ili ufaulu wa wanafunzi kuweza kusoma kwa kuwelewa hasa masomo ya sayansi kwanini kumekuwa na upungufu wa wataalamu wa sayansi.

mkurungenzi wa direct aid sheikh  ayman  muhammed  kamaldin  amesema katika mwaka huu wanafunzi wa skuli hiyo wanatarajia kufanya vizur   kwa walivyojitayarisha na kuahidi kusaidia katika mambo ya uongozi wa skuli hiyo.

Mwalimu kuu wa skuli hiyo  ndg abdalah nasosr amsema katika skuli hiyo wanaomba kupatiwa udhamini wa mikopo kwa wanafunzi ili waze kujiunga naelimu ya juu  na kushukuru wazazi na walimu kwa kuhakikisha skuli hiyo inarudisha heshima kubwa nakuweza kuto wanafuzi wengi ingawa hawakuwezakuto daraja la kwanza lakini daraja la pili ni wengi.