WALIMU WA SKULI ZA MSINGI NA MAANDALIZI KUBUNI MBINU ZA KUFUNDISHIA

Wizara ya elimu na mafunzo ya amali imewataka walimu wa skuli za msingi na maandalizi kubuni mbinu za kufundishia ili kuongeza kiwango cha elimu nchini pamoja na kufuata maadili ya uwalimu na nchi kwa ujumla.
Akizungumza na walimu wa msingi na maandalizi wa wilaya ya kaskazini “a” naibu waziri wa wizara hiyo mmanga mjengo mjawiri amesema walimu lazima wabadilike kwa kujiendeleza kwa masomo pamoja na kubuni mbinu kadhaa za kufundishia zikienda sambamba na kuheshimu maadili ya uwalimu na ya nchi kwa ujumla.
Wakichangia maada walimu hao wamesema tatizo la kukosa nauli kwa walimu wanaoishi mbali na skuli wanazosomesha linawasababishia walimu hao baadhi ya siku kutofika skuli walizopangiwa.
Akitoa ufafanuzi wa suala la nauli kwa walimu wanaoishi mbali na skuli zao mkurugenzi idara ya elimu maandalizi na msingi bibi safia ali rijali amesema utaratibu wa awali wa kuwasaidia nauli walimu hao ulikuwa unafanywa na wizara lakini kwa utaratibu wa sasa maombi yote ya nauli kwa walimu yanapelekwa utumishi hivyo amewataka walimu kuwa na uvumilivu kwani wizara inafanya juhudi za kutatua tatizo hilo.