WALIMU WAKUU KUFANYIWA TATHMINI SERA YA ELIMU HASAWANAFUNZI WA DARASA LA NNE LA SITA KUFUATIA CHANGAMOTO ZINAZOONEKANA

Walimu wakuu wa skuli za wilaya ya mkoani wameomba kufanyiwa tathmini sera ya elimu hasa katika mfumo wa mitihani ya wanafunzi wa darasa la nne la sita kufuatia  changamoto zinazoonekana kwa wanafunzi wa madarasa hayo.

Hayo yamebainika  wakati wauchangiaji  kwa walimu hao katika mkutano wa siku moja   kati ya walimu wakuu wa wilaya ya mkoani na  naibu waziri wa wizara ya elimu  zanzibar  mh.mmanga mjengo mjawiri  ikiwa ni  katika ziara  yake  ya kuonana na  walimu hao.

Wamesema mbali na changamoto nyingi zinazowakabili  ikiwemo ya uhaba wa walimu  pia wameitaka wizara  kuweza kuifanyia tathmini  sera  hiyo  kwani  sasa imekuwa ni mzigo  kwao .

Nae naibu waziri wa wizara  ya elimu  na mafunzo ya amali zanzibar mh.mmanga mjengo mjawiri amesema  licha ya sababu zinazotajwa  kwa mfumo wa ufanyaji wa mitihani kwa wanafunzi wa darasa la nne  na sita   ni kutokana na kutoelezwa vizuri kwa mfumo huo kwa jamii  na  ndio maana mwiitiko wa ufanyaji wa mitihani hiyo kwa wanafunzi wa darasa  la nne ukawa mdogo  na kuwataka walimu hao  waendelee kutoa elimu  juu ya mitihani  hio kwa jamii.

Mapema akisoma taarifa ya elimu ya wilaya ya mkoni afisa elimu wa wialaya  hiyo nd,seif mohammed seif akielezea  hali ya matokeo  katika mwaka  wa 2016  amesema katika wilaya hio haikuwa nzuri kiufaulu ambapo   matokeo ya  kidato cha nne  yanaonyesha  wanafunzi asilimia  4.4  ndio walifaulu  u kilinganishwa na mwaka 2015  huku darasa  la sita  walioingia michipuo  ni wanafunzi 41  kati ya wote waliyofanya mtihani   ambapo  matokeo hayo  ni yakuhuzunisha ,kusononesha na  kukatisha tamaa kwa  kila mmoja.