WALIMU WAMETAKIWA KUWA NA TABIA YA KUJITATHMINI MARA KWA MARA ILI KUJUA MAFANIKIO NA MATATIZO

Walimu wametakiwa kuwa na tabia ya kujitathmini mara kwa mara ili kujua mafanikio na matatizo ya ufundishaji kwa wanafunzi ili kuongeza kiwango cha Elimu hapa nchini.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh: Mmanga Mjengo mjawir amesema ili kukuza kiwango cha elimu na kufikia malengo ni vyema kuwekwa  utaratibu huo wa kujitathmini katika skuli utasaidia  kutatua tatizo la kufeli wanafunzi

akizungumza na walimu wa Skuli za maandalizi na msingi wa wilaya ya kaskazni B katika kikao cha kujadili matatizo ya elimu amewataka walimu hao kujiendeleza kielimu ili kukuza taaluma yao.

baadhi ya walimu walioshiriki kikao hicho wameiomba Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali kutoa  kipaumbele cha Ajira kwa Walimu wanaojitolea kwani ni miongoni wanaotoa mchango mkubwa kwa wanafunzi.

mkuu wa wilaya ya kaskazini b Issa Juma Ali ametoa nasaha zake kwa walimu hao hasa katika kuimarisha sekta hiyo ya Elimu.