WALIMU,WAZAZI NA WAZEE WAMETAKIWA KUWA NA USHIRIKIANO KATIKA MALEZI YA WATOTO

 

Walimu,wazazi na wazee wametakiwa kuwa naushirikiano katika malezi ya watoto ili wakue katika  maadili mema.

Akizungumza katika kuwakabidhi zawadi wanafunzi walio fanya vizuri katika mashindao ya kuhifadhi  qur-an yalioandaliwa na rehmet-fi-sabililah kada wa ccm bi yasmi haluu amesema misingi mizuri ndio silaha ya kumtukuza molla na ndiyo itakayomfikisha peponi kila muislamu.

Ameahidi kuendelea kuwasaidia walimu na wanafunzi wa vyuo vya qur-an katika kuendeleza mambo mema ili kuzalisha mashekh na  wanazuoni wengi visiwani hapa .

Wakitoa shukrani zao wanafunzi yaliokabidhiwa zawadi hizo wameushukuru uongozi wa rehmat-fi-sabililah kwa kuwaandalia mashindano hayo pamoja na kutowa zawadi ambazo zitakuwa chachu ya kupenda kusoma zaidi kitabu cha mungu kur -an.