WALINZI WANAOLINDA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA KUTUMIA LUGHA NZURI KWA WATU WANAOKWENDA KUANGALIA WAGONJWA

Naibu waziri wa afya mh; harousi ali suleiman Amewasisitiza walinzi wanaolinda hospitali ya Mnazi mmoja kutumia lugha nzuri kwa
Watu wanaokwenda kuangalia wagonjwa.
Akifungua mafunzo ya namna ya kumshuhulikia mgonjwa kwa walinzi wa hospitali hiyo mh harous amesema ni makosa kumtolea mgonjwa maneno yasio faa kwani kufanya hivyo wanaipa sifa mbaya serikali ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa hospitali hiyo
Nae msaidizi mkuu wa ulinzi abubakar hassan amesema kutokana na malalamiko mengi yanayotolewa na wagonjwa mafunzo hayo yatasaidia kutaleta mabadiliko na utendaji bora wa kazi zao
Kwa upande wake mkurugenzi wa utawala na uwendeshaji katika hospitali ya mnazi mmoja abubakar khamis hamad amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ushirikiano mzuri baina ya walinzi na wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo…
Mafunzo hayo yanayohusu namna ya kumshuhulikia mgonjwa yameandaliwa na hospitali kuu ya mmnazimmoja na kuwashirikisha walinzi wa hospitali hiyo…