WAMESHAURI KUJENGWA DARAJA KATIKA ENEO LA BWAWA LA MWANAKWEREKWE

 

Wananchi mbali mbali  wameshauri kujengwa daraja    katika eneo la bwawa la mwanakwerekwe ili maji yanayokatisha njia   hiyo yaweze kupita kwa urahisi  wakati wa  mvua  kubwa zinaponyesha.

Wamesema suala la kujengwa mtaro katika eneo hilo haitakuwa suluhisho  kutokana na wingi  wa  maji yanayopita  katika maeneo hayo ya mwanakwerekwe.

Malalamiko  ya wananchi hao yamekuja kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jana jioni na  kutokea  uharibifu  wa barabara  ya mwanakwerekwe huku vyombo  vya moto vikipita kwa tabu.

Wamesema  iwapo  kutajengwa  daraja  kubwa  kutaweza kudhibiti     wingi wa maji yanayokatisha  njia  kutoka maeneo jirani na kushuka  hadi    katika  bwawa hilo..

Wamesema  ujenzi huo wa daraja pia utasaidia  wakaazi jirani kuhama hama katika maeneo yao wanayoishi kama ilivozoeleka katika msimu wa mvua za masika