WAMILIKI NA WASIMAMIZI WA MAHOTELI NA SEKTA NYENGINE KUFUATA SHERIA

 

 

Waziri wa wizara ya uwezeshaji vijana wazee ajira wanawake  na watoto mh bi Mouldine Castico amewataka wamiliki na wasimamizi wa mahoteli na sekta nyingine binafsi kufuata sheria na maagizo yatolewayo na  serikali kuu katika kuwapatia wafanyakazi wao stahiki husika ikiwemo upandishwaji wa mishahara .

Amesema hivi karibuni serikali ilipandisha kiwango cha chini cha mshahara na kufikia laki tatu badala ya laki na hamsini na kuzitaka taasisi nyingine kurekebisha mishahara ya wafanyakazi wao

Mh castico ameyasema hayo huko hoteli ya pemba misali wakati akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa hoteli hiyo kujua changamoto zinazowakabili ikiwemo mishahara na usalama kazini

Awali afisa mdhamini wizara ya uwezeshaji vijana wazee ajira wanawake na watoto pemba bi khadija khamis rajab amesema ziara hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya serikali kuzipitia kila taasisi kuangalia maslahi ya wafanyakazi kutumikishwa na stahiki wanazopewa .

naye meneja wa hoteli ya pemba misali zahran juma ali amemtaka waziri huyo kuishauri serikali kuhusu usafiri wa wageni kuja zanzibar kwani malipo wanayotoa huishia kisiwani   unguja pekee na kushindwa kufika na kisiwa cha pemba jambo ambalo linawakosesha wageni kutembelea hoteli yao.