WAMILIKI WA HOSPITALI BINAFSI KUTOA TIBA SAHIHI KWA WAGONJWA

 

 

Wamiliki wa dispensary za mkoa wa mjini magharibi wametakiwa kuwa na ushirikiano ili kutoa tiba sahihi kwa wagonjwa.

Mratibu wa ukaguzi wa hosptali binafsi makame khamis amezitaka dispensasry hizo kufuata sheria ili kuepuka kufungiwa kutoa huduma

Ameeleza kuwa katika ukaguzi huo wamezifungia baadhi ya dispensary mpaka watakaporekebisha kasoro  zao

Amesema endapo watashindwa kufanya hivyo watanyanganywa leseni pam,oja na kutozwa faini ili iwe fundisho kwa wengine

Kwa upande wake mkaguzi wa dawa nassoro silemani amewataka wamiliki wa dispensary hizo kutunza mazingira na vifaa  wanavyotumia kwa kuvihifadhi vizuri katika sehemu salama

Jumla ya  disepensary 16 za mkoa wa mjini  magharibi imefanyiwa ukaguzi na bodi ya  ukaguzi wa hosptali binafi