WAMILIKI WA SKULI BINAFSI WAMESISITIZWA KUFUATA MISINGI YA ELIMU ILI KUKIDHI HAJA YA SERIKALI KATIKA KUWAPATIA ELIMU WATU WAKE.

Wamiliki wa skuli binafsi wamesisitizwa kufuata misingi ya elimu sambamba na wizara ya elimu ili kukidhi haja ya serikali katika kuwapatia elimu watu wake.
Akizungumza katika siku ya wazazi katika skuli ya kareem islamic afisa elimu mkoa wa mjini magharibi mwalimu khatib tabia amesema skuli hizo zikifuata misingi hiyo lengo la skuli binafsi kuisaidia serikali litafikiwa.
Amesema skuli hizo zimetoa mchango mkubwa katika kupunguza wingi wa wanafunzi katika madarasa na kuongezeka kwa maendeleo ya taifa.
Mwalimu khatib tabia katika mkutano huo amewaagiza wamiliki wa skuli binafsi pamoja na kuwekea katika elimu ni vyema wakajenga majengo halisi ya skuli na kuacha tabia ya kutumia nyumba za kawaida kuwa ni skuli.
Katika taarifa ya skuli hiyo ya kareem islamic wameiomba serikali kurahisisha utaratibu wa upatikanaji wa vitabu vya kufundishia ili kuleta fanisi na maendeleo ya elimu.
Skuli ya kareem islamic iiliyopo fuoni mambo sasa ina zaidi
Wanawafunzi 200 inafundisha kuanzia hatua ya awali na msingi.