WAMILKI WA MASHAMBA YA MIKARAFUU KUHAKIKISHA WANAITUNZA MIKARAFUU HIYO

 

Mkuu wa wilaya ya kaskazini b ndugu rajab ali rajabu amewataka wamilki wa mashamba ambayo yamepandwa mikarafuu kuhakikisha wanaitunza mikarafuu hiyo ili kuongeza pato la nchi kupitia zao hiloAmeeleza hayo wakati wa shughuli za upandaji wa mikarafuu katika mashamba ya donge ikiwa na lengo la kurudisha haiba ya vijiji hivyo katika ukulima wa karafuuShughuli hiyo iliyoshirikisha viongozi mbalilmbali akiwemo mwakilishi wa jimbo la donge muheshimiwa khalid muhammed , vijana himahima,  pamoja na watendaji mbalimbali wa wilaya ya kaskazini bmkuu wa wa wilaya ya kaskazini b  ndugu rajabu amesema zao la karafuuu ni miongni mwa zao linaloingizia serikali mapato ambayo yamekuwa yakisaidia katika kutoa huduma mbalimbali za kijamiiMwakilishi wa jimbo la donge ndugu khalid muhhammed amesema atahakikisha anaandaa kamati maalum ya kushughulikia mikarafuu hiyo ili iweze kukua na lengo la serikali liweze kufikiaAfisa kilimo kutoka idara ya kilimo ndugu badru kombo amesema kitendo cha serikali kutoa mikarafuu kwa wananchi wake ni kitendo cha kuungwa mkono kwani zao hilo ni zao lenye utajiri kwa wakulima wenye kufuata taratibu za kilimo hichoJumla ya mikarafuu kumi na tano elfu inatarajiwa kupandwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya kaskazini b ambapo hadi sasa mikarafuu elfu sita imeshapandwa