WANACHAMA PSPF KUPATA MIKOPO KUPITIA BENKI YA CRDB

 

Wanachama wa mfuko wa pensheni wa pspf  wataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya crdb baada ya kuzinduliwa  mpango huo kati ya taasisi hizo mbili.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mpango huo , mkurugenzi mkuu wa pspf, adam mayingu , amesema mpango wa kutoa mikopo ulianza tangu desemba 2014 kupitia taasisi nyingine za kifedha.
amesema pspf na benki ya crdb wamekubaliana kushirikiana kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo ikiwemo ya elimu katika ngazi mbali mbali, mkopo wa kuanzia maisha na mkopo wa viwanja.

Amefafanua kuwa lengo la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto zake