WANACHAMA WA CCM KUENDELEA NA MOYO WA KUJITOLEA ILI KUPIGA HATUA KATIKA MAENDELEO.

 

Makamu mwenyekiti wa umoja wa wanawake ccm tanzania uwt mhe: thuwaiba  edington kisasi  amewataka  wanachama wa chama hicho wa mkoa wa kusini unguja kuendelea na moyo  wa kujitolea ili mkoa  huo  uzidi  kupiga hatua katika maendeleo.Akizungumza na wanachama   wa   uwt   mkoa wa kusini    unguja ikiwa  ni  miongoi mwa ziara zake za  kujitmbulisha   baada  ya  kuchaguliwa kua makamo mwenyekiti  wa umoja huo  kisasi  amesema imani ,hamasa na uzalendo  ndio ngao muhimu  ya  kulinda   ushindi  wa chama  hicho  ambayo  pia  itasaidia kuongeza  idadi ya wanchama.

Naibu katibu mkuu  wa  umoja  huo   mh: salama   aboud talib akizungumzia  fursa  za wanawake  katika  umoja  huo   ndani   ya mkoa  wa kusini naibu katibu mkuu  wa  umoja  huo   mh: salama   aboud talib amesema  wanawke wana  nafasi kubwa  katika  kuhakikisha  wanaibua  njia   zitakazoimarisha  miradi  ya  maendeleo   walioianzisha ikiwemo  ujasiriamali na kilimo  cha mboga mboga  ambayo imeanzishwa kwa lengo  la  kjiongezea  kipato  katika familia zao.