WANACHAMA WA KIKUNDI CHA KUWEKA NA KUKOPA CHA SUBIRA NJEMA WAMEANZA KUFAIDIKA

 

 

wanachama wa kikundi cha kuweka na kukopa cha subira njema kiliopo meli nne taveta wameanza kufaidika na na mafao waliyokusanya na kugawana fedha ili kujikimu kimaisha.

hafla kuvunja kisanduku na kugawana fedha hizo imefanyika mbele ya maafisa wa mfuko wa maendeleo ya jamii tanzania tassaf ambapo wanachma 14 wa kikundi hicho amekabidhiwa shilingi laki mbili na arubaini elfu, ambazo zimetokana na makusanyo ya shilingi milioni tatu.

mwenyekiti wa kikundi hicho bi asha suleiman ali,  na baadhi ya wanachama wanaelezea maendeleo ya kikundi chao.

afisa ushirika wilata ya magharibi ‘a’ nd kassim ali ni msimamizi wa kutoa mafunzo na ushauri kwa vikundi vya ushirika.

mbali na kuweka na kukopa, kikundi cha subira njema , kinajiendeleza kwa kilimo cha mboga mboga katika bonde la kijitoupele, ikiwa ni sehemu ya kisaidizi kwa mahitaji madogo madogo kwa wanachama hao.

naibu sheha pamoja na afisa kutoka tassaf wameelezea kuridhishwa na uendeshaji wa kikundi hicho cha kinamama.