WANACHAMA WA SACCOS YA MAENDELEO YA ELIMU WAMEUTAKA USHIRIKA HUO KUHARAKISHA UPATIKANAJI WA MIKOPO

Wanachama wa saccos ya maendeleo ya elmu t d s wameutaka ushirika huo kuharakisha upatikanaji wa mikopo kwa wanachama wake ili iwasaidie kujiendeleza kimaisha.
Wanachama hao wametoa ushauri katika mkutano mkuu wa saba wa chama hicho uliofanyika skuli ya sekondari ya lumbumba .
Wamesema wamejiunga na saccos hiyo ili iwasaidie kujiendeleza sambamba na kuondoa changamoto zinazowakabili lakini endapo hawatapata mikopo kwa wakati ushirika huo hautakuwa na mana kwao.
Akiwasilisha ripoti ya fedha ya ushirika huo kiongozi mmoja wa sacos hiyo amesema zaidi ya shilingi milioni mia saba na sitini zilitarajiwa kukusanywa mwaka 2017.
Sacos hiyo ya walimu ina jumla ya wanachama mia tisa na sitini na tisa hadi hivi sasa ambapo lengo la kuanzishwa kwake ni kuwaendeleza walimu.