WANAFAMILIA WA KAYA MASIKINI WAMELALAMIKIA HALI YA UCHELEWESHWAJI WA FEDHA NA VITENDEA KAZI

 

Wanafamilia wa kaya masikini wanaojishughulisha na ukulima wa kilimo cha mpunga wa kutegemea mvua katika bonde la muyuni b kupitia mradi wa tasaf wamelalamikia hali ya ucheleweshwaji wa fedha na vitendea kazi kutofika kwa wakati.Wanafamilia hao wametoa malalamiko yao kufuatia ziara ya mkuu wa mkoa wa kusini unguja mhe hassan khatib hassan baada ya kuangalia maendeleo ya mradi huo katika bonde hilo.

Wamesema kwa kipindi cha miezi mitatu sasa tangu kuanza kwa shughuli za matayarisho ya bonde hilo hawajapatiwa malipo yoyote wala vitendea kazi  hivyo wameuomba uongozi unaosimamia mradi huo kuharakisha upatikanaji wa malipo ili waweze kukamilisha kazi hiyo kwa ufanisi  Nae mkuu wa mkoa huo amewapongeza wanakaya hao kwa juhudi nzuri waliyofikia licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu na kusisitiza kwamba  serikali itaendelea kuwatafutia wananchi fursa mbali mbali waweze kuondokana na umasikini.jumla ya kaya masikini 72 za kijiji cha muyuni zinatarajiwa kunufaika na mradi huo wa tasaf utakapokamilika.