WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA ZANZIBAR KUTUMIA ELIMU WALIOIPATA ILI KUCHOCHEA MAENDELEO YA TAIFA LAO.

 

Waziri Biashara na Viwanda Mhe, Balozi Amina Salum Ali amewataka Wanafunzi wa chuo cha utumishi wa Umma Zanzibar kutumia elimu walioipata ili kuchochea maendeleo ya taifa lao.

Amesema wakati wa kufanyakazi kwa mazoweya umekwisha hivyo amesisitiza umuhimu kwa wananchi kutafuta elimu kwa kila jambo kwani elimu ni siri ya maendeleo.

balozi amina ameeleza hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho katika hafla ya kukabidhiwa vibaraza vya kusomea masomo ya ziada njee ya majengo ya chuo hicho vilivyojengwa kwa msaada wa kampuni wa pen royal .

Amewahimiza wanafunzi hao kuwa na mtazamo wa mbali zaidi kwa kusoma sana na hatimae kuiwezesha  Zanzibar kuwa na wataalamu wa kutosha watakasadia ukuaji wa uchumi wa kati.

Mkurugenzi wa kampuni ya pen royal inayojishughulisha na utalii amesema ipo haja ya kwa serikali kupunguza urasimu kwa kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza na kuwasikiliza matatizo yanayokwamisha  miradi yao ya uwekezajii.

Wanafunzi wa chuo hicho wameipongeza juhudi za kampuni ya Pen Royal kwa kuwajengea sehemu ya kusomea  na kutowa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiga mfano huo.

Vibaraza hivyo vya kusomea  vitakuwa vinaweza kuchukuwa idaddi ya wanafunzi 48 kwa wakati moja katika muda wa ziada wa masomo.