WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR UNIVERSITY (ZU) KUSIKITISHWA NA HATUA YA KUFUTWA KWA KOZI

 

Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha zanzibar university  (zu) wameelezea kusikitishwa  na hatua ya kufutwa kwa kozi walizozichagua na kupelekea wanafunzi wengine kuacha kuendelea na masomo chuoni hapo.

Wakizungumza na zbc wamesema uamuzi huo uliochukuliwa na uongozi wa chuo wa kuzifuta kozi hizo na kuwapangia kujiunga na kozi nyengine kinyume na matarajio yao hatua hiyo imewapa usumbufu kwa kiasi kikubwa.

Zbc  baada ya kupata habari hizo kutoka kwa wanafunzi  ilikwenda katika ofisi za msaidizi naibu makamo mkuu – taaluma, zu dr. Moh’d makame haji kwa ajili kupata ufafanuzi kuhusiana na suala hilo la kufutwa kwa baadhi ya kozi chuoni hapo.

Aidha jambo jengine walilolalamikia  wanafunzi  hao   ni kupandishwa  kwa ada  kwa  mwaka huu hali iliyopelekea kuwaongezea mzigo kwa vile walikwisha jipangia utaratibu wa matumizi.

Dr moh’d pia akalitolea ufafanuzi suala hilo.

Chuo kikuu cha zanzibar university (zu) kina zaidi ya miaka 20 tokea kuanzishwa kwake na kina kozi zaidi ya 19 ambazo zinatolewa chuoni hapo kozi ambazo zimetolewa katika muhula huu wa masomo  ni tano(5) ikiwemo public administration, islamic bank and finance, language arabiq , swahili ,mass communication, na it with education –geography.