WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU WASISITIZWA KUTUMIA FURSA

 

Wanafunzi wa elimu ya juu wasisitizwa kutumia fursa wanazozipata katika vyuo mbalimbali hasa yanayohusiana na masuala ya uongozi ili kuwa mfano  bora wa viongozi wa baadae.

Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi mh: ayoub akiuzngumza katika sherhe ya serikali ya wanafunzi wa chuo cha utawala wa umma (zipaso) uongozi unahitaji uelewa hivyo  fursa ya kujifunza masula hayo ni kujiweka tayari na utendaji pindi wanapokuwa watumishi hasa kwenye taasisi za umma..

Mkurugenzi wa chuo cha utawala wa umma  bi harusi ali masheko  amesema kupitia serikali ya wanafunzi  ya zipaso  chuo kimepiga hatuwa kubwa kielimu pamoja na kushiriki shughuli mbali mbali za kijamii .

Akisoma risala mwanafunzi  hudhaima  mbarak amesema  licha ya chuo hicho kufikia maendeleo mazuri  bado kinakabiliwa na changamoto  kadhaa  ikiwemo  upungufu wa vitabu  na kutokua na uzio  kwa ajili ya kulinda  mali  za chuo  na usalama  mzuri wakiwa chuoni hapo.