WANAFUNZI WA SKULI ILI KUONGEZA KASI YA UFAULU WA MASOMO

 

Naibu waziri wa elimu namafunzo ya amali mh  mmanga mjengo mjawiri amesema  walimu maafisa wa elimu wazazi pamoja  na kamati za skuli  wanawajibu mkubwa kusimamia wanafunzi wa skuli ili kuongeza kasi ya ufaulu wa masomo yao  kwa kutumia mbinu  za kisasa  za ufundishaji kwa walimu.

mh mmanga ameyasema hayo huko makunduchi  wakati wa kujadili kikao  cha pamoja  kilichowashirikisha walimu wakuu masheha  mafisa  pamoja na kamati za  skuli  za mkoa wa kusini unguja.

Amesema  walimu wananafasi kubwa  katika kuhakikisha wanafunzi wanafaulu  kwa kiwango kizuri  na kuelewa matatizo ya wanafunzi hao.

nao walimu hao wa skuli hizo za wilaya  wa kusini wameahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa na wakuu wa wizara ya elimu .

wakati huo huo  naibu waziri huyo amepokea walimu kumimna sita kutoka nchi ya nageri kwa  kuja zanzibar kufundisha masomom ya sayansi ikiwemo physics na hesabu ili kupunguza uhaba wa walimu katika masomo ya sayansi na kuwataka walimu hao kutumia njia   nzuri katika ufundishaji wao.

naye mkurugezi kutoka nchi ya nigeria  mr  afolabi  oduniyi amesema wapo tayari kuwafundisha wanafunzi hao  kwa kufuata sheria  na kanuni zilizowekwa kwa makubaliano.