WANAFUNZI WAMETAKIWA KUTAFUTA MBINU TOFAUTI ZA KUJIFUNZA

 

Akizungumza katika mashindano ya utendenezaji wa ndege kwa wanafunzi wa skuli mbali za Zanzibar beit Ras.

Mkurugenzi Utawala na Utumishi Nd Omar Ali Bhai amesema vijana wengi wanapomaliza masomo yao huwa hawana mbinu za kujitafutia maisha hivyo ni vyema kuwa na mwamko mzuri wa kusoma na kujitambua nini wanafanya kabla na baada ya kumaza masomo yao.

Hata hivyo Bhai amesema Wizara yake ina kabiliwa na changa moto kubwa ya ukosefu ya walimu wa Sayansi hivyo ufaulu wa wanafunzi hao ndio utakao fanya kupata walimu bora hapa Zanzibar.

Amewataka walimu wa Sayansi kuongeza juhudi katika kuwasomesha wanafunzi na kuzidisha ushieikiano kwa wadau kwani Wizaya inadhamini michango inayotolewa na Tasisi mbali mbali katika kuchangia maendeleo ya Elimu Nchini.

Mratibu wa Mradi wa Masomo ya  Sayansi Elimu na Ufundi Ali Mohamed Abdalla kutoka Zanzibar Milele Foundation amesema malengo ya Mradi ni kuongeza idadi ya wataalamu wa Sayansi  ili kufikia mikakati iliyo bora.

Nao washiriki wa mashindano hayo walipata nafasi ya kujieleza jinsi walivyotengeneza Ndege zao.

Jumla ya skuli kumi na tano zimeshiriki katika utengenezaji wa Ndege kwa kutumia plastic  na washindi wa watatu wa mwanzo watapata nafasi ya kusafiri kwa Ndege znz to dar.