WANAJESHI WA MAREKANI NA KOREA KUSINI KUGUNDUA UFYATUWAJI WA MAKOMBORA

Kiongozi wa korea kaskazini kim jong un amesema nchi yake inakaribia kufikia lengo lake la kulingana nguvu za kijeshi na marekani.
Shirika la habari la serikali la korea kaskazini knca limetoa matamshi hayo ya kim siku moja baada ya wanajeshi wa marekani na korea kusini kugundua ufyatuwaji wa makombora yake.
majaribio hayo ya pyongyang yamezidi kuibua hofu ya kikanda huku china ikisema imejiandaa kutekeleza vikwazo vya umoja wa mataifa.
aidha balozi wa china nchini marekani ameitaka marekani kuacha kuitisha korea kaskazini na badala yake itafute namna nyinge za kupata sululu.