WANAJESHI WAASI WAMUUA RAIA IVORY COAST

Wanajeshi wanaofanya uasi Ivory Coast kutokana na mgogoro wa malipo wamemuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa baada ya kutumia risasi kutawanya umati wa watu waliojitokeza jana kuandamana kupinga uasi huo wa Jeshi katika mjii wa Bouake ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo. Wanajeshi hao walifunga barabara nyingi za mji huo kutokana na mzozo wa malipo ambao bado haujatatuliwa. Alhamisi wiki iliyopita, baaadhi ya wanajeshi hao walionekana katika kituo cha televisheni wakikutana na rais Alassane Ouattara na kuachana na matakwa yao ya kulipwa. Wanajeshi hao waasi waliyateka makao makuu ya jeshi na wizara ya ulinzi katikati ya mji mkuu Abidjan Ijumaa na kusababisha kuzuka mvutano mkali na wanajeshi wa kikosi cha rais. Mkuu wa majeshi wa Ivory Coast amesema operesheni ya kijeshi imeanzishwa ili kurejesha hali ya utulivu baada ya wimbi hilo la uasi