WANAKIKUNDI WA BAU GROUP WAMEFURAHISHWA NA HATUA YA SERIKALI KUWAJALI KATIKA KUWAWEZESHA KIUCHUMI.

 

 

 

Wanakikundi wa bau group kilichopo karakana  wamefurahishwa na hatua ya serikali kuwajali katika  kuwawezesha kiuchumi. Kamera ya biashara na uchumi  ilikutana na wanakikundi hao walipotembelewa na kamati ya maendeleo ya wanawake habari na utalii ya baraza lawawakilishi kutaka kujua  na kuona maendeleo ya kikundi hicho  jinsi kilivyopiga hatua  katika  mradi wao wa kusaga nafaka.Akizungumza na wanakikundi hao mwenyekiti wa kamati  hiyo mh ali suleiman shihata  amesema wamefurahishwa na hatua waliyoichukua wanakikundi hao  kutokana na fedha walizopatiwa na serikal.i

Mwenyekiti wa ushirika  huo amesema  kupatiwa kwa pesa hizo  wameweza kumiliki  mashine tatu za kusagia nafaka  na kuwaingizia kipato kinachokidhi  mahitaji yao.Mbali ya mafanikio hayo  wanakabiliwa na tatizo la uhaba nyenzo za kufanyia kazi amoja na udogo wa ofisi yao