WANANACHI WAMETAKIWA KUCHUKUWA TAHADHARI KUJIKINGA NA KIPINDUPINDU

wananachi wametakiwa kuchukuwa tahadhari katika kujikinga na maradhi ya kipindupindu kwani kumebainika wadudu wanaosababisha maradhi hayo wapo kwa asilimia kubwa.
mkurugenzi wa mamlaka ya kujikinga na maafa ali juma akizungumza katika mkutano wa kutathmini hali ya maradhi hayo amesema jitihada zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kuikumbusha na kuielimisha jamii juu ya kujikinga na maradhi hayo ambapo tatizo la uelewa mdogo unasababisha kuripuka kwa maradhi hayo kwa kila mwaka.
mkugugenzi wa kinga na elimu ya afya dk. fadhili mohammed amesema licha ya kuibuka kwa maradhi ya kipindupindu kwa muda mrefu lakini zanzibar imeweza kusifiwa katika kutokomeza maradhi hayo ikilinganishwa na nchi nyengine.
mwakilishi mkaazi wa who ghirmay andemichael amesema katika uchungu uliofanywa na shirika hilo umegundua asilimia kubwa ya maradhi hayo yanatokana na kunywa maji yasio salama.
jumla ya vifo 68 vilitokea zanzibar mwaka jana kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.