WANANCHI KUACHA KUJENGA NYUMBA AU KUPANDA MITI YA KUDUMU KATIKA MAENEO YA UWEKEZAJI

Serikali imewataka wananchi kuacha kujenga nyumba au kupanda miti ya kudumu katika maeneo ambayo yametengwa kwa uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti huko chamanangwe na micheweni na waziri wa ardhi, nyumba, maji, na nishati, mh salama aboud talib chini ya jopo la mawaziri wane waliotumwa na serikali kushughulikia mizozo ya wananchi waliojenga na kupanda miti ya kudumu katika maeneo ya uwekezaji.

Mheshimiwa salama amesema ifikie wakati wananchi kutambua kwamba maeneo ya uwekezaji hayaruhusiwi kufanyiwa kitu chochote mbadala ya kilichoelekezwa na serikali hivyo sibusara kwa mtu kujichukulia eneo bila ruhusa kutoka mamalaka husika.

Awali sheha wa shehia ya kiuyu minungwini yahya salim amir ambayeeneo lake la chamanangwe linalomilikiwa na wizara ya kilimo limejengwa nyumba tano na kutumika kwa kilimo amewashauri wananchi kukubali kufanyiwa tathmini ya malizao na kuhama ili kuiwachia serikali kufanya shughuli zake

Naye mkuu wa wilaya ya micheweni salama mbarouk khatib amesema watahakikisha kuona maeneo hayo yaliyotengwa haya tumiwi vibaya .

Miongoni mwa mawaziri walihudhuria katika kazi hiyo ni waziri wa biashara, viwanda na masoko balozi amina salim ali, waziri wa habari na mambo ya kale mheshimiwa mahmoud thabit kombo na waziri wa ujenzi, mawasiliano na usafirishaji mheshimiwa sira ubwa mwamboya

 

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App