WANANCHI KUACHA TABIA YA KUCHIMBA MCHANGA KIHOLELA

 

Mkuu wa wilaya ya magharibi ‘b’ silima haji  amekemea   tabia ya  baadhi ya  wananchi kuacha tabia ya  kuchimba   mchanga kiholela   hali inayosababisha uharibifu   wa   mazingira   ikiwa   ni   pamoja   na   mafuriko   wakati   wa   mvua Akizungumza   wakati   akikagua   maeneo   ya   kinuni   na   maungani yalioharibika  kwa kuchimbwa   mchanga    amesema   hali   hiyo   haikubaliki    na  kwamba serikali  ya  wilaya hiyo   itawachukulia   hatua   wale   wote   wanaoendeleza vitendo   hinyo   kinyume   na   utaratibu   ikiwa  ni  pamoja   na kukamatwa   kwa   gari   zao    za  ng’ombe  ..

ndugu  silima   amewataka   vijana   wanaojishuhulisha   na vitendo   hivyo   kuacha   mara   moja   na  badala  yake   kusubiri   mpango   wa   serikali   ya   mkoa    ya   kuwapatia   njia   mbadala   za kufanya   biashara   ili   kuwacha   vitendo  hivyo.

Katika  hatua    nyengine   mkuu  wa  wilaya  ya  magharibi ‘b’  silima haji   amesimamisha   ujenzi   na   uuzwaji   wa   viwanja   katika   eka ya ndugu  salum  saidi  kindi iliopo  fuoni   ambayo inadaiwa kuwa na mgogoro wa umiliki   na bibi  arafa  mussa.

Amewataka   wadai   hao   kupeleka   hati   na   vielelezo   vyao   vyote   vya   umuliki    wa   maeneo   hayo   katika   ofisi   ya   wilaya hiyo   ili   kuweza   kutoa   maamuzi   sahihi   ya  mgogoro  huo uliodumu  kwa takribani  miaka  mitatu   sasa.