WANANCHI KUHESHIMU MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali moh’d shein amewataka wananchi na waumini wa dini ya kiislamu kuheshimu mwezi mtukufu wa ramadhani unaotarajiwa kwanza hivi karibuni .
Akizungumza kwa niaba yake katika kongamano la kukaribisha mwezi huo waziri wa nchi ofisini ya rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora mh haroun ali suleiman amesema mwezi huo ni mwezi kwa waislam kuzingatia kufanya yale yote yanayompendeza mwenyezi mungu na kwamba waislam wote wanapaswa kuaingatia hayo.
Aidha amewahimiza waislam kutumia mwezi huo vizuri na kutoa sadaka kwa wale wenye uwezo kama vitabu vinavyoeleza.
Mufti mkuu wa zanzibar salehe omar amesema waislam wana wajibu wa kuzingatia mambo yote mema katika mfungo huo.
Nae imam qasim alghan kutoka marekani amewasisitiza waislam kushikana katika kuitetea dini hiyo na badala yake kuepukana na migongano miongoni mwao.
Kongamano hilo la siku moja kwa mara ya kwanza loimefanyika zanzibar katika kuukaribisgha mwezi mtukufu wa ramadhani.