WANANCHI KUIUNGA MKONO ZANZIBAR HEROES KWA JITIHADA WALIZOZIONESHA

 

Timu ya taifa ya zanzibar heroes yaahidiwa zawadi kemkem  wakati itakaporejea nchini na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dr ali muhammed shein , huku akitoa ahadi ya zawadi nyengine maalum iwapo vijana hao watarudi na kombe la michuano ya mataifa ya afrika mashariki cecafa challenge cup.

Hayo yameelezwa leo na waziri wa habari utalii  utamaduni na michezo zanzibar, rashid ali juma wakati akiwasilisha salamu za rais kwa  timu ya zanzibar heroes na wananchi wa zanzibar  ikiwa ni kuwaunga mkono vijana hao kwa jitihada walizozionesha hadi sasa.

Amesema  miongoni mwa maagizo ya rais wa zanzibar ni kuhakikisha timu ya taifa ya zanzibar heroes inarejea  nchini kwa usafiri wa ndege, ijapo kuwa wachezaji hao  wamesema wangelipenda kutumia usafiri walioutumia hapo awali walipoanza mashindano hayo huko machakos nchini kenya.

Nae katibu mkuu wa wizara ya habari utalii utamaduni na michezo, omar hassan kingi pia amewasilisha salamu za rais kwa kusema kuwa  wananchi wa  zanzibar, wanaombwa  kushiki kikamilifu katika kuipokea timu ya taifa ya zanzibar heroes mara tu itakaporejea nchini katika viwanja vya  ndege  vya abeid aman karume.

Zanzibar imefanikiwa kwenda fainali ya kombe la mataifa ya afrika mashariki cecafa challenge baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi, uganda jana  jioni  katika uwanja wa moi mjini kisumu, kenya.
Zanzibar sasa itakutana na wenyeji,  kenya kwenye mchezo wa fainali jumapili katika uwanja wa kenyatta mjini machakos, nchini kenya, hayo yakiwa ni marudio ya mchezo wa kundi a, uliomalizika kwa sare ya 0-0 desemba 9.